KISWAHILI DARASA LA TANO
nukuu za mtaala mpya
1SURA YA KWANZA
1.0 KUWASILIANA KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI
1.1 Kuendeleza mazungumzo katika miktadha mbalimbali
a) Kutumia msamiati katika kusimulia matukio, habari na vitu mbalimbali
kwa kujiamini
KUSIMULIA MATUKIO
Nini maana ya msamiati?
Ni mkusanyiko wa maneno yanayotumiwa katika lugha fulani ili kufikisha
maana au mawazo
Kwa kifupi, msamiati ni hazina ya maneno ya lugha
Mfano wa misamiati na maana zake
1. Katili – kutokuwa na huruma
2. Mwambao – sehemu ya nchi iliyokaribu na bahari
3. Ghala – jengo la kuhifadhia vitu au bodhaa
4. Kiuka – fanya isivyostahili
5. Dafina – vitu vya thamani vilivyofichwa katika ardhi
6. Shubiri – kitu chenye uchungu sana
7. Shangazi – dada wa baba
8. Bikira – mwanamke au msichana ambaye hajawahi kushiriki tendo la
ndoa
9. Jabali – mwamba mkubwa pia hutumika kumaanisha mtu mwenye nguvu
na jasiri
10. Hitilafiana – kutoafikiana katika kufanya mambo mbalimbali
11. Wahaini – watu ambao wapo tayari kuidhuru nchi yao
12. Fukara – mtu maskini au mwenye uwezo mdogo wa kiuchumi
13. Samba – enea kila mahali
14. Kongwe – kilicho cha zamani sana
15. Utepe – Kamba laini mara nyingi ya mapambo
16. Mvinyo – kinywaji cha kienyeji cha kilevi chenye chachu ya zabibu
17. Uhaba – ukosefu wa kutosha wa kitu
18. Mwangaza – nuru au mwanga unaoruhusu kuona vizuri
19. Takrima – upendo au zawadi inayotolewa kwa heshima au ukarimu
20. Dhahiri – bila ya kuficha
21. Ujasiri – uwezo wa kukabiliana na hatari au hofu
222. Hodari – mtu mwenye ujuzi au uwezo mkubwa
23. Ushirikiano – kufanya kazi Pamoja kwa lengo moja
24. Ustadi – uwezo wa kufanya jambo vizuri au kwa ujuzi
25. Ubora – kiwango cha juu au cha thamani
26. Mwongozo – maelekezo au kielelezo kinachosaidia kufanya jambo
27. Dhihaka – mchezo wa kejeli kwa kumdharau mtu
28. Hila – njia au mbinu ya udanganyifu, ujanja wenye nia mbaya au ulaghai
Soma hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata
Mtengo wa vitendawili
Nzige, Panya na Kiwavi waliishi msituni Pamoja na Kipepeo, Nyoka, Ndege,
Mjusi na Mzee Ngedere. Nzige, Panya na Kiwavi walikuwa marafiki
walioshirikiana kwa mambo mabaya. Mara nyingi marafiki hawa walivamia
mashamba ya Binadamu na kufanya uharibifu wa mazao.Walileta kero kubwa
Binadamu alitumia mbinu nyingi ili kuwaangamiza viumbe hao lakini mbinu
zake hazikufua dafu.Siku moja, Mzee Ngedere alikwenda kwa Binadamu
kuomba kazi ya kuwaangamiza Nzige, Panya na Kiwavi
Binadamu alicheka sana kwa kumdharau Mzee Ngedere.Mzee Ngedere
akasema “Usinichekeshe “. Binadamu akamjibu , “Mimi nimehagaika miaka
nenda miaka rudi sijaweza kuwakamata, wewe utawezaje na uzee wako,”
Mzee Ngedere alieleza
“Utahitaji malipo gani? “ Binadamu aliuliza.Mze Ngedere akamjibu kuwa
atajilipa kwa kuchukua mazao anayoyataka shambani kwa binadamu.
Binadamu alimruhusu Mzee Ngedere. Mzee Ngedere akaandaa tangazo kuwa
kutakuwa na shindano la kutegua vitendawili.A liahidi zawadi ya shamba na
ghala la chakula kizuri kwa atakayetegua kitendawili chake kwa usahihi
Nzige, Panya na Kiwavi walilipata tangazo hilo wakiwa wamejibanza
mafichoni. Nzige akawauliza wenzake, “Rafiki zangu, hivi mnaujua utamu wa
vitendawili? “Kiwavi akajibu, “Mimi ninajua >Vitendawili ni vitamu kuliko
hata chakula.Twendeni nikawaoneshe uhodari wangu wa kutegua vitendawili.”
Panya naye hakuwa nyuma. Akasema , “Hilo shamba na ghala lazima nivipate
mimi.
3Nitafaidi utamu wa vitendawili na nitajipatia ghala la vyakula vizuri. Lazima
nife kishujaa kupta ushindi huu.”
“Hebu tusiandikie mate na wino ungalipo. Twendeni tukashindane.”Kiwavi
aliwahimiza wenzake. Wote wakachapa mguu kuelekea jukwaa la kufanyia
shindano. Wanyama na wadudu wengine walipowaona Panya na wenzake
wakiingia ukumbini kwa maringo, Waliwashangilia kwa nguvu.Nzige, Panya na
Kiwavi wakajipanga nyuma na kuwa wa mwishomwisho ili vitendawili vigumu
zaidi viishe
Kipepeo, Nyoka, Ndege na Mjusi ndo waliotangulia .Wote wakashindwa
kutegua vitendawili vya mzee Ngedere. Nzige, Panya na Kiwavi hawakuacha
nyuma maringo yao ikiwa ni moja ya silaha ya ushindi wao.Hatimaye ,
ikawadia zamu ya Kiwavi. Alijinyonganyonga kwa madaha akapanda jukwaani
na kusubiri kitendawili .
“Kitendawili”Mzee Ngedere alisema. Kiwavi akajibu “Tega.”
“Nikikutanana na adui yangu nanyong’onyea.Nipatie jib una maana yake.”Mzee
ngedere alitega na kuomba jibu `Kiwavi alichemsha bongo akajibu haraka bila
kupoteza muda, “Jiubu lake ugonjwa.Maana yake ni kuwa ugonjwa
umefananishwa na adui, ugonjwa ni adui mkubwa wa viumbe.Binadamu
akikutana na ugonjwa, anakuwa mnyonge. Hata sisi viumbe wengine vivyo
hivyo.” Mzee Ngedere akamwambia, “Umepata!”
Panya alisogea akarukaruka kwa mikogo jukwaani. Mzee Ngedere akamtegea
kitendawili chake, “Adui tumemzingira lakini hatumuwezi.”Panya akajibu
“jibu lake ni moto.Maana yake ni kuwa hata tukiwa wengi kiasi gani hatuwezi
kukabiliana na joto la moto tunaouoata.Moto umefananishwa na adui ambaye
watu wamemzunguka kana kwamba wanamshabulia, “Mzee Ngedere
akamwambia, “Umepata
Baada ya panya kutegua kitendawili, Nzige akawa wa mwisho kutegua
kitendawili chake.Mzee Ndegere akatega akisema, “Ukumbuu wa babu
mrefu.”Nzige aliyainua mabawa yake kwa mbwembwe na kutoa sauti y anti nti
nti! Kisha akajibu, “Njia! Maana yake ni kwamba njia ni ndefu kama ukumbuu.
Kitendawili hiki kinafananisha urefu wa njia na mshipi.”
Mzee Ngedere aliwapongeza marafiki hao watatu kwa kutegua vitendawili na
kuvipatia maana zake kwa usahihi.Akawaomba waende kwenye chumba cha
mapumziko ili wasubiri hatua ya pili .Waliingia kwenye chumba mlimokuwa na
chakula kizuri kilichoandaliwa na mzee Ngeder.Wakaanza kula. Siku za mwizi
ni arobaini, na ujanja mwingi mbele kiza. Walipogutuka wakajikuta
4wamekwishafungiwa humo, huku nje binadamu akiwatizama kwa dhihaka.
Wakadhani ni kiinimacho. Kumbe mzee Ngedere alikuwa amekula njama
kuwakamata kwa hila na hilo lilikuwa gereza la waharibifu wa mazao
Binadamu alimshukuru Mzee Ngedere kwa msaada wake akisema , “Ama kweli
umadhaniaye ndiye kumbe siye! Mze Ngedere naye alimshukuru Binadamu
kwa kumpatia nafasi, kisha akarejea mlimani.Kama malipo ya kazi hiyo, Mzee
Ngedere Ngedere wakati mwingine huenda kwenye mashamba ya binadamu na
kula mazao
Zoezi 01 ufahamu
Eleza kwa ufupi matukio yaliyotokea katika hadithi uliyoisoma
Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?
Binadamu alijaribu kuwaangamiza Panya na wenzake kwa muda gani
bila mafanikio?
4. Taja zawadi mbili amabazo Mzee Ngedere aliahidi kumpa mshindi wa
kutegua vitendawili
5. Nani aliyewambia wenzake wasiandikie mate na wino ungalipo?
BACK TO SCHOOL ONLINE MATERIAL
Karibu ujipatie
1. 2. 3. 1.scheme of work| – azimio la kazi
2.Lesson plan – Andalio la somo
3.Lesson Notes – Nukuu za somo
4.Log Book – Shajara
5.Holiday Package
Karibu kwa huduma nzuri uaminifu na uhakika Zaidi
Piga 0694361925 WhatsApp 0627064154
5