Nukuu za somo la sayansi darasa la Tano
NUKUU ZA SAYANSI MTAALA MPYA
Nukuu za mtaala mpya
DARASA LA TANO
2026
SURA YA KWANZA
MFUMO WA MMENG’ENYO WA CHAKULA
Dhana ya mfumo wa mmenge’nyo wa chakula
1Mmeng’enyo wa chakula ni mchakato wa kibailojia ambapo chakula
huvunjwavunjwa kuwa chembechembe ndogo zenye virutubisho ambavyo
mwili unaweza kufyonza.
Mmeng’enyo wa chakula hufanyika katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni mkusanyiko wa ogani au viungo vya
mwili wa binadamu vinavyohusika na kuvunjavunja chakula kuwa
chembechembe ndogo zenye virutubisho zinazoweza kufyonzwa na kutumiwa
na mwili
Ili kudumisha afya ya mfumo huu, ni muhimu kula mlo kamili kwa wakati
sahihi, kunywa maji ya kutosha, kuepuka kula vyakula vyenye mafuta au sukari
kwa wingi ili kuimarisha afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mbali na binadamu, wanyama wengine pia wana mifumo ya kumeng’enya
chakula inayotofautiana kutokana na aina ya vyakula wanavyokula
Sehemu za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula unahusisha ogani mbalimbali ambazo
hufanya kazi kwa Pamoja ili kurahisisha uvunjwaji wa chakula. Mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula wa binadamu huanzia kwenye kinywa hadi kwenye
njia ya haja kubwa. Mfumo huu unajumuisha njia ya chakula, ogani na tezi
zinazofanya kazi Pamoja
Sehemu kuu za njia ya chakula ni
a. Kinywa
b. Koromeo
c. Umio
d. Mfuko wat umbo
e. Utumbo mwembamba
f. Utumbo mpana
Utumbo mwembamba unajumuisha duodeni na iliamu. Vilevile, utumbo mpana
unajumuisha koloni, puru na njia ya kutolea haja kubwa
Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula pia unajumuisha tezi za mate na zile
zinazopatikana katika mfuko wat umbo. Vilevile, baadhi ya ogani kama ini,
2kongosho na kibofu nyongo zina tezi zinazozalisha vimeng’enya vinavyotumika
katika kumeng’enya chakula
Kinywa
Ni sehemu ya kwanza ambapo chakula huingia. Hapa chakula hutafunwa na
kuchanganywa na mate ili kirahisishe kumezwa na kuanza kumeng’enywa.
Koromeo
Ni njia ya kupitishia chakula kutoka kinywa kwenda umio. Husaidia kuelekeza
chakula kisiingie kwenye njia ya hewa.
Umio
Ni mrija unaosafirisha chakula kutoka koromeo hadi mfuko wat umbo kwa
kutumia misuli inayojikaza na kulegea.
Mfuko wa tumbo
Hapa chakula huchanganywa na aside na vimeng’enya ili kivunjwe vipande
vidogo na kuwa uji laini.
3Utumbo mwembamba
Ndiyo sehemu kuu ya mmeng’enyo na ufyonzwaji wa virutubisho kama sukari,
protini na mafuta kwenda kwenye damu.
Utumbo mpana
Husaidia kufyonza maji na madini yaliyokusanya na kukaza kinyesi kabla ya
kuelekezwa kwenye puru.
Koloni
Ni sehemu ya utumbo mpana inayokusanya na kukaza kinyesi kabla ya
kuelekezwa kwenye puru.
Puru
Ni sehemu ya kuhifadhia kinyesi kwa muda mfupi kabla ya kutolewa nje ya
mwili.
Njia ya kutolea haja kubwa
Ni tundu la mwisho ambapo kinyesi hutolewa nje ya mwili.Kinyesi ni mabaki
ya chakula ambayo hayakumeng’enywa na kufyonzwa na mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula
Kasoro katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
kasoro katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni hali inayoathiri utendaji
wa kazi wa kawaida wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kufanya iwe
vigumu kwa mwili kumudu kumeng’enya na kufyonza chakula ipasavyo.
Kasoro hizo zinaweza kuwa za kimaumbile, kurithi au zinazotokana na mtindo
wa Maisha na lishe duni. Baadhi ya kasoro za mfumo wa mmeng’enyo wa
chakula ni kama zifuatazo
1. Kupata choo kigumu
Ni hali ambayo kinyesi huwa kigumu sana na kikavu kasoro hii husababishwa
na ulaji wa vyakula vyenye kiwango cha chini cha nyuzinyuzi, kutokunywa
maji ya kutosha na ukosefu wa mazoezi ya mwili.Pia, matatizo ya kiafya kama
vile utendaji duni wa utumbo mpana husababisha kupata choo kigumu
Njia za kuzuia
Hali hii huzuiwa kwa kula vyakula vyenye nyunzinyuzi za kutosha kama vile
matunda na mbogamboga, kunywa maji ya kutosha na kufanya mazoezi mara
kwa mara
42. Kuvimbiwa
Ni hali ambayo mfuko wat umbo hujaa, kuwa mgumu au kuvimba, mara nyingi
hutokanana na mkusanyiko wa gesi katika mfuko wat umbo. Tatizo la
kuvimbiwa husababishwa na kula chakula kingi kupita kiasi , kula vyakula
vinavyosababisha gesi au tumbo kutovumilia baadhi ya vyakula
Dalili za mtu kuvimbiwa nit umbo kuuma, kuhisi tumbo kujaa gesi na kupiga
mbweu.wakati mwingine gesi hiyo huwa na harufu kali na mbaya
Njia za kuzuia
Ili kuzuia unapaswa kula chakula kwa kiasi na kutafuna polepole ili kupunguza
kiasi cha hewa inayomezwa. Vilevile, kunywa maji ya kutosha ili kurahisisha
mmeng’enyo wa chakula katika mfuko wat umbo. Kupunguza ulaji wa vyakula
vyenye gesi kama vile maharage na unywaji wa vinywaji vyenye gesi kama vile
sod. Pia, ulaji wa matunda na mboga za majani huzuia kuvimbiwa
3. Kiungulia
Ni hali ya kuhisi moto au maumivu kifuani au kooni yanayosababishwa na aside
ya tumbo kupanda juu, hali inayochangiwa na kula vyakula vyenye mafuta au
viwango vikali, kula sana kisha kulala Pamoja na kunywa pombe au kahawa
nyingi
Njia za kuzuia
Unaweza kuzuia kiungulia kwa kula chakula taratibu ili kurahisisha
mmmeng’enyo wa chakula. Pia kula chakula kidogokidogo lakini mara kwa
mara pia kupunguza viungo na mafuta mengi.Epuka kulala mara tu baada ya
kumaliza kula.Vilevile epuka kufanya mazoezi au kazi ngumu muda mfupi
baada ya kula chakula. Hali ya kiungulia ikizidi ni vyema kupata ushauri wa
kitabibu
fano wa pili, kitendo kinarudiwa mpaka jambo fulani litokee (kihusika kiguse
ukingo) kwenye mfano wa tatu kitendo kinarudiwa bila kikomo hadi mchezo
uishe
5BACK TO SCHOOL ONLINE MATERIAL
Karibu ujipatie
1.scheme of work| – azimio la kazi
2.Lesson plan – Andalio la somo
3.Lesson Notes – Nukuu za somo
4.Log Book – Shajara
5.Holiday Package
Karibu kwa huduma nzuri uaminifu na uhakika Zaidi
Piga 0694361925 WhatsApp 0627064154
67891011121314151617………..………………………. THE END ……………………………
18