February 19, 2026

WatuCrash

📚 Education & Learning Hub (Primary + Secondary)

Kiswahili

KUSIMULIA MATUKIO

  1. KUWASILIANA KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI
  2. Kuendeleza mazungumzo katika miktadha mbalimbali
  3. Kutumia msamiati katika kusimulia matukio, habari na vitu mbalimbali kwa kujiamini

Nini maana ya msamiati?

Ni mkusanyiko wa maneno yanayotumiwa katika lugha fulani ili kufikisha maana au mawazo Kwa kifupi, msamiati ni hazina ya maneno ya lugha

Mfano wa misamiati na maana zake

  1. Katili – kutokuwa na huruma
  2. Mwambao – sehemu ya nchi iliyokaribu na bahari
  3. Ghala – jengo la kuhifadhia vitu au bodhaa
  4. Kiuka – fanya isivyostahili
  5. Dafina – vitu vya thamani vilivyofichwa katika ardhi
  6. Shubiri – kitu chenye uchungu sana
  7. Shangazi – dada wa mama
  8. Bikira – mwanamke au msichana ambaye hajawahi kushiriki tendo la ndoa
  9. Jabali – mwamba mkubwa pia hutumika kumaanisha mtu mwenye nguvu na jasiri
  10. Hitilafiana – kutoafikiana katika kufanya mambo mbalimbali
  11. Wahaini – watu ambao wapo tayari kuidhuru nchi yao
  12. Fukara – mtu maskini au mwenye uwezo mdogo wa kiuchumi
  13. Samba – enea kila mahali
  14. Kongwe – kilicho cha zamani sana
  15. Utepe – Kamba laini mara nyingi ya mapambo
  16. Mvinyo – kinywaji cha kienyeji cha kilevi chenye chachu ya zabibu
  17. Uhaba – ukosefu wa kutosha wa kitu
  18. Mwangaza – nuru au mwanga unaoruhusu kuona vizuri
  19. Takrima – upendo au zawadi inayotolewa kwa heshima au ukarimu
  20. Dhahiri – bila ya kuficha
  21. Ujasiri – uwezo wa kukabiliana na hatari au hofu
  22. Hodari – mtu mwenye ujuzi au uwezo mkubwa
  23. Ushirikiano – kufanya kazi Pamoja kwa lengo moja
  24. Ustadi – uwezo wa kufanya jambo vizuri au kwa ujuzi
  25. Ubora – kiwango cha juu au cha thamani
  26. Mwongozo – maelekezo au kielelezo kinachosaidia kufanya jambo
  27. Dhihaka – mchezo wa kejeli kwa kumdharau mtu
  28. Hila – njia au mbinu ya udanganyifu, ujanja wenye nia mbaya au ulaghai

Soma hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata

Mtengo wa vitendawili

Nzige, Panya na Kiwavi waliishi msituni Pamoja na Kipepeo, Nyoka, Ndege, Mjusi na Mzee Ngedere. Nzige, Panya na Kiwavi walikuwa marafiki walioshirikiana kwa mambo mabaya. Mara nyingi marafiki hawa walivamia mashamba ya Binadamu na kufanya uharibifu wa mazao.Walileta kero kubwa

Binadamu alitumia mbinu nyingi ili kuwaangamiza viumbe hao lakini mbinu zake hazikufua dafu.Siku moja, Mzee Ngedere alikwenda kwa Binadamu kuomba kazi ya kuwaangamiza Nzige, Panya na Kiwavi

Binadamu alicheka sana kwa kumdharau Mzee Ngedere.Mzee Ngedere akasema “Usinichekeshe “. Binadamu akamjibu , “Mimi nimehagaika miaka nenda miaka rudi sijaweza kuwakamata, wewe utawezaje na uzee wako,”

Mzee Ngedere alieleza

“Utahitaji malipo gani? “ Binadamu aliuliza.Mze Ngedere akamjibu kuwa atajilipa kwa kuchukua mazao anayoyataka shambani kwa binadamu.

Binadamu alimruhusu Mzee Ngedere. Mzee Ngedere akaandaa tangazo kuwa kutakuwa na shindano la kutegua vitendawili.A liahidi zawadi ya shamba na ghala la chakula kizuri kwa atakayetegua kitendawili chake kwa usahihi

Nzige, Panya na Kiwavi walilipata tangazo hilo wakiwa wamejibanza mafichoni. Nzige akawauliza wenzake, “Rafiki zangu, hivi mnaujua utamu wa vitendawili? “Kiwavi akajibu, “Mimi ninajua >Vitendawili ni vitamu kuliko hata chakula.Twendeni nikawaoneshe uhodari wangu wa kutegua vitendawili.”

Panya naye hakuwa nyuma. Akasema , “Hilo shamba na ghala lazima nivipate mimi.

Nitafaidi utamu wa vitendawili na nitajipatia ghala la vyakula vizuri. Lazima nife kishujaa kupta ushindi huu.”

“Hebu tusiandikie mate na wino ungalipo. Twendeni tukashindane.”Kiwavi aliwahimiza wenzake. Wote wakachapa mguu kuelekea jukwaa la kufanyia shindano. Wanyama na wadudu wengine walipowaona Panya na wenzake wakiingia ukumbini kwa maringo, Waliwashangilia kwa nguvu.Nzige, Panya na Kiwavi wakajipanga nyuma na kuwa wa mwishomwisho ili vitendawili vigumu zaidi viishe

Kipepeo, Nyoka, Ndege na Mjusi ndo waliotangulia .Wote wakashindwa kutegua vitendawili vya mzee Ngedere. Nzige, Panya na Kiwavi hawakuacha nyuma maringo yao ikiwa ni moja ya silaha ya ushindi wao.Hatimaye , ikawadia zamu ya Kiwavi. Alijinyonganyonga kwa madaha akapanda jukwaani na kusubiri kitendawili .

“Kitendawili”Mzee Ngedere alisema. Kiwavi akajibu “Tega.”

“Nikikutanana na adui yangu nanyong’onyea.Nipatie jib una maana yake.”Mzee ngedere alitega na kuomba jibu `Kiwavi alichemsha bongo akajibu haraka bila kupoteza muda, “Jiubu lake ugonjwa.Maana yake ni kuwa ugonjwa umefananishwa na adui, ugonjwa ni adui mkubwa wa viumbe.Binadamu akikutana na ugonjwa, anakuwa mnyonge. Hata sisi viumbe wengine vivyo hivyo.” Mzee Ngedere akamwambia, “Umepata!”

Panya alisogea akarukaruka kwa mikogo jukwaani. Mzee Ngedere akamtegea kitendawili chake, “Adui tumemzingira lakini hatumuwezi.”Panya akajibu

“jibu lake ni moto.Maana yake ni kuwa hata tukiwa wengi kiasi gani hatuwezi kukabiliana na joto la moto tunaouoata.Moto umefananishwa na adui ambaye watu wamemzunguka kana kwamba wanamshabulia, “Mzee Ngedere akamwambia, “Umepata

Baada ya panya kutegua kitendawili, Nzige akawa wa mwisho kutegua kitendawili

chake.Mzee Ndegere akatega akisema, “Ukumbuu wa babu mrefu.”Nzige aliyainua mabawa yake kwa mbwembwe na kutoa sauti y anti nti nti! Kisha akajibu, “Njia! Maana yake ni kwamba njia ni ndefu kama ukumbuu. Kitendawili hiki kinafananisha urefu wa njia na mshipi.”

Mzee Ngedere aliwapongeza marafiki hao watatu kwa kutegua vitendawili na kuvipatia maana zake kwa usahihi.Akawaomba waende kwenye chumba cha mapumziko ili wasubiri hatua ya pili .Waliingia kwenye chumba mlimokuwa na chakula kizuri kilichoandaliwa na mzee Ngeder.Wakaanza kula. Siku za mwizi ni arobaini, na ujanja mwingi mbele kiza.

Walipogutuka wakajikuta wamekwishafungiwa humo, huku nje binadamu akiwatizama kwa dhihaka. Wakadhani ni kiinimacho. Kumbe mzee Ngedere alikuwa amekula njama kuwakamata kwa hila na hilo lilikuwa gereza la waharibifu wa mazao

Binadamu alimshukuru Mzee Ngedere kwa msaada wake akisema , “Ama kweli umadhaniaye ndiye kumbe siye! Mze Ngedere naye alimshukuru Binadamu kwa kumpatia nafasi, kisha akarejea mlimani.Kama malipo ya kazi hiyo, Mzee Ngedere Ngedere wakati mwingine huenda kwenye mashamba ya binadamu na kula mazao

Zoezi 01 ufahamu

  1. Eleza kwa ufupi matukio yaliyotokea katika hadithi uliyoisoma
  2. Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?
  3. Binadamu alijaribu kuwaangamiza Panya na wenzake kwa muda gani bila mafanikio?
  4. Taja zawadi mbili amabazo Mzee Ngedere aliahidi kumpa mshindi wa kutegua vitendawili
  5. Nani aliyewambia wenzake wasiandikie mate na wino ungalipo?

Zoezi 02 Msamiati

Eleza maana ya maneno yafutayo kisha tunga sentensi mbili kwa kila neno

  1. Kiwavi
  2. Jibanza
  3. Dhihaka
  4. Kiinimacho
  5. Hila
  1. Maringo
  2. Gutuka

Zoezi 03 Nahau na misemo

Eleza maana y anahau na misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye hadithi uliyoisoma

  1. Chapa mguu
  2. Kata tamaa
  3. Chemsha bongo
  4. Kula njama
  5. Leta kero
  6. Uzee ni dawa
  7. Miaka nenda miaka rudi

Zoezi 04 vitendawili

Tegua nae leza matukio katika vitendawili vifuatavyo

  1. Mtungini mwangu hamuingii kata
  2. Wakikkua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo
  3. Kondoo wetu ananyama nje na Ngozi ndani
  4. Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke
  5. Akitembea huringa hata akiwa hatarini
  6. Fuu fuu funua, fuu fuu funika
  7. Wali wa mama mtamu
  8. Wana wa mfalme ni wepesi kujificha

Zoezi 05 mazoezi ya lugha Kanusha sentensi zifuatazo Mfano

Mzee Ngedere ana busara Mzee Ngedere hana busara

  1. Panya, Nzige na Kiwavi walishirikiana kwa mambo mema
  2. Binadamu ataweza kumkamata Panya na wenzake
  3. Viumbe hawa hupenda mafumbo
  4. Mjusi atashinda shindano la vitendawili
  5. Mzee Ngedere alikula njama kuwakamata wezi
  6. Panya alisogea jukwaani kwa mikogo
  7. Nzige na binadamu ni marafiki

Zoezi 06

Kamilisha habari hii kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia manno yaliyomo kwenye kisanduku

Watoto walikuwa (i) na kuoglea kwenye dimbwi karibu na nyumbani kwao.Wlizama na kuibuka kwenye yale maji (ii) . Miili yao (iii) matope.Haikuwa rahisi (iv) sura zao. Bibi Loshi alipokuwa anapita pale,

  1. wale watoto. “Loo! Nyie watoto mtaleta balaa! Maji hayo yana
  2. Wengi.Tokeni haraka. “wale watoto walitoka (vii) nguo zao. Bibi Loshi (viii) , “Humo ndani mna wadudu wanaosababisha (ix) , homa ya matumbo na magonjwa mengine. Ondekeni wajukuu zangu.”wale watoto (x)

. Pia, Bibi Loshi (xi) akaendelea na safari yake.

Zoezi la 07

Panga sentensi katika mtiririko sahihi

  1. Siku ile ilikuwa ya furaha mno, kwani ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kupanda mlima
  2. Likizo ilikuwa nzuri sana kwani tulikula mahindi ya kuchoma na kuchemsha
  3. Sote tulipanda mlima bila shida, lakini ilipofika wakati wa kushuka ilikuwa taabu sana
  4. Tulishindwa kushuka kwa miguu, tukatambaa mithili ya nyoka
  5. Mpwa alitutembeza sehemu mbalimbali za vivutio kama vile milima yenye miamba mikubwa
  6. Tulifika chini tukiwa hoi lakini sote tulikuwa tumefurahi kupanda mlima
  7. Likizo ya mwezi wa sita nilienda kwa mpwa wangu wilayani Mbulu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *