MUONGOZO WA KISWAHILI DARASA LA SABA
MUONGOZO WA KISWAHILI DARASA LA SABA
LUGHA YA
KIFASIHI
Methali, nahau, vitendawili,
misemo na mafumbo
Maana na mifano mbalimbali
Kutumia maandishi kaitka
kuandaa mofimu mbalimbali
– Methali
– Nahau
– Vitendawili
– Misemo
– Mafumbo
Kutumia maandishi katika
kuwasiliana kulingana miktadha
mbalimbali
MISAMIATI
Maana ya msamiati na mifano yake
– Visawe
– vitawe
– vinyume
– vikembe
– Misamiati ya kazi
– Misamiati ya mavazi
– Misamiati ya chakula
– Misamiati ya wanayama/mifugo
Ushairi
Ushairi
USHAIRI
Maana ya shairi
Aina za shairi
KUONESHA
UWELEWA
(UTUNGAJI)
a. Mashiri ya kimapokeo
b. Mashairi guni, mapingiti, masivina au kisasa
Ngonjera, nyimbo, tenzi
Hotuba
Maana ya hotuba
Muundo wa hotuba
Sifa za hotuba
Aina za hotuba
– Mahubiri- Hotuba za ksiasa na kiserikali
– Mihadhara aumasomo darasani
Risala
Maana ya risala
Muundo wa risala
Barua
Maana ya barua
Barua za kirafiki
Muundo wa barua za kirafiki
Barua za kiofisi au kibiashara
Muundo wa barua za kiofisi
Insha
Mana ya insha
Aina za insha
– Insha za wasifu
– Insha za hoja
Muundo wa insha
Matangazo
Maana ya matangazo
– Kuandika matangazo mbali mbali kwa
kuzingatia taratibu za uandishi
– Kuandika kumbukumbu za mikutano
Kadi za mialiko
Maana ya kadi ya mwaliko
Muundo wa kadi ya mwaliko
Ufahamu
Maana ya ufahamu
Aina za ufahamu
– Ufahamu wa kusikiliza
– Ufahamu wa kusoma
Namna ya kubaini kicwa cah habariSifa ya kichwa cha habari
Mbinu za kujibu maswali ya ufahamu
Kamusi
Maana ya kamusi
Aina za kamusi
Muundo wa kamus
Kamusi
AINA ZA MANENO
Kubaini aina za maneno katika sentensi
Neno – ni mkusanyiko wa sauti zinazotamkwa na kuandikwa pamoja na kuleta maana.
Aina saba za maneno kama ifuatavyo.
1. Nomino/Jina (N).
2. Kiwakilishi (W).
3. Kitenzi (T)Kielezi (E).
4. Kivumishi (V).
5. Kiungnishi (U).
6. Kihisishi (Kiingizi (I).
7. Kihusishi.
NOMINO
Ni maneno yanayotaja majina ya watu, vitu na mahali. Pia nomino ni maneno makuu yanayotawala kirai
nomino au kikundi nomino.
Mfano
Morogoro, Juma, Asha, Kilimanjaro.
Mti, Daftari, Kiti, Kikombe.
AINA ZA NOMINO.
i. Nomino za pekee.
ii. Nomino za kawaida.
iii. Nomino za jumla au jamii.
iv. Nomino za dhahania.
v. Nomino za wingi.
(i)Nomono za pekeeNi majina maalumu yanayotaja vitu au watu wenye maumbile ya kipekee. Majina haya kila
yanapoandikwa huanzia kwa herufi kubwa.
Majina ya watu binafsi.
Mfano:
Juma, Zuena, John, Hamis, Hawa, Adam.
Majina ya siku za juma.
Mfano:
Jumatatu Jumanne, Jumatano.
Majina ya mezi.
Mfano:
Januari, Machi, Juni
Majina kama Kijiji, Wilaya, Tarafa, Kata, Mkoa, Nchi.
Mfano:
Mtakuja, Rombo, Mbezi, Saranga, Sigida, Tanzania, Asia.
Majina ya milima.
Mfano:
Kilimanjaro, Meru.
Majina ya mto, maziwa na bahari.
Mfano:
Ruvuma, Malagarasi, shamu, Victoria, Tanganyika.
Mfano wa sentensi.
Dar -es -salaam kuna msongamano wa magari sana.
Oliver amesafiri.
Anna yupo shuleni.
Mbezi ipo Dar- es –slaam.
Rombo ni wilaya yetu.
Juma nacheza mpira vizuri.
(ii)Nomino za kawaida
Ni majina ya jumla ya vitu vya kawaida vyenye umbile.
Mfano:
Wanyama, wadudu, mimea, viatu, nyumba.
Chui wakali wamekuja.
Simba ni mnyama mkali.
Kipepeo amekamatwa na chura.
Kuku ni ndege.
(iii)Nomino za jumla au jamii.
Ni nomino zinazotaja au kujumuisha vitu au watu wengi katika kundi moja.
Mfano:
Genge, kikosi, kamati, mkutano, chama, halmashauri, bunge,katoni na korija.
– Jeshi la Tanzania limeenda Kenya.
– Kamti imeundwa vizuri.
– Chama chetu kinatoa mkopo.
– Bunge limevunjwa leo.
(iv)Nomino za dhahania.
Ni majina ya kufikirika ambayo hayaonekani, hayagusiki wala hayakamatiki.
Mfano:
Njaa, uchovu, joto, upendo, baridi, shetani, malaika, usingizi, wivu, uvivu, upepo.
– Uvivu siyo mzuri.
– Shetani ashikiki kabisa.- Malaika alimtokea samweli.
– Njaa siyo nzuri kabisa.
(v)Nomino za wingi.
Ni majina mbayo dhana yako ipo kaitka wingi lakini hayana umoja wake.
Mfano:
Maji, maziwa, mwasiliano, mafuta, madhumuni, mate, matakwa, mafua, maoni, machozi.
Machozi yanamtoka juma.
Maoni ya Asha ni mazuri.
Mafuta yameletwa.
Madhumuni yetu ni kufanya vizuri kwenye mtihani wetu wa mwisho.
Maji yetu yamemwagika.
VIWAKILISHI (W).
Ni maneno yanayotumika badala ya nomino.
AINA ZA VIWAKILISHI.
a. Viwakilishi vya sifa.
b. Viwakilishi vya nafsi.
c. Viwakilishi vya idadi.
d. Viwakilishi vya kuonesha/mahali.
e. Viwakilishi vya kumiliki.
f. Viwakilishi vya kuuliza.
g. Viwakilishi vya kurejesha.
h. Viwakilishi vya A-unganifu.
(a)Viwakilishi vya sifa.
Viwkailishi vya sifa hutaja watu, kitu au jambo Fulani.
Mfano:
Wanene, mkali, mcheshi, wafupi, mweusi, mrefu.
– Wanene wapite mbele.
– Wafupi wasimame mbele.
– Mcheshi amekuja.
– Mweusi aje nyuma.
(b)Viwakilishi vya nafsi.
Viwakilishi vya nafsi hutumika kubainisha nafsi ya mzungmzaji.
Kiwakilishi cha nafsi kimegawanyika katika makundi mawili.
a. Viwakilishi vya nafsi huru.
b. Viwakilishi vya nafsi viambata.
(a)Viwakilishi vya nafsi huru.
Haya ni maneno mazima yanayoweza kusimama pekee yake bila kuambatanishwa katika neno au mzizi
wa neon.
Kwa mfano
Nafsi Umoja Uwingi
I Mimi Sisi
II Wewe Ninyi / nyingi
III Yeye Wao
– Mimi sijalima shamba.- Sisi niwageni kutoka Kenya.
– Wewe ni mfanyabiashara.
– Wao wanasoma kitabu.
(b)Viwakilishi vya nafsi viambata.
Hizi ni mofimu tegemezi au vipande vya maneno vinavyoambatanishwa kaitka neno au mzizi wa neno
jingine ili kudokeza ua kutaja nafsi husika.
Kwa mfano:
NAFSI UMOJA WINGI
I Ni Tu
II U M
III A Wa
Nitacheza mpira kesho.
Tutaimba nyimbo nzuri.
Utasoma kitabu kesho.
Mmecheza mpira vizuri.
Anapika ugali.
Walikimbia jana.
(c)Viwakilishi vya idadi.
Viwakilishi vya idadi huwakilisha idadi au hesabu ya vitu au watu.
Mfano:
Manne, maelf, vingi, kumi, wachache.
– Mawili yamegongana.
– Vichche vimepatikana.
– Wane wamekamatwa.
– Watano wamekimbia.
– Wengi hawakula.
(d)Viwakilishi vya kuonesha/mahali.
Viwakilishi vioneshi husimama badala ya nomino lakini hudokeza umbali au ukaribu wa kitu, mtu au
jambo Fulani kutoka kwa mzungumzaji.
Mfano
Haya, Wale, Mle, Yule, Hapa, Hichi, Hili, Hicho.
Hili limeiva.
Yule ni mvivu.
Hicho ni kitamu sana.
Wale wameandika.
Pale pana maji mengi.
(e)Viwakilishi vya kumiliki.
Viwakilishi vimilikishi huonesha umiliki wa kitu au jamii Fulani.
Mfano:
Zenu, changu, chao, yao, chake, chetu, kwao.
– Yangu imepotea.
– Yenu imepatikana.
– Yao imepotea.- Chenu kimeiva
– Change sikioni.
(f)Viwkailishi vya kuliza.
Haya ni maneno yanayowakilisha nomino na huwa na kazi ya kuuliza swali.
Mfano:
Nani, lini, ngapi, yupi, kipi?
– Kipi kimepotea?
– Nani amekuja?
– Ngapi zimechukuliwa?
– Lini unakuja?
(g)Viwakilishi vya kurejesha.
Ni maneno au viwakilishi vinavyorejea nomino ambayo haikutajwa.
Mfano
Aliyemaliza aondoke.
Ambacho kimenunuliwa.
Ambalo halioni.
Ambaye ametaga.
Ambao wameoza.
(h)Viwakilishi vya A- unganifu.
Mfano:
– Wa meru umeungua.
– Ya mapambano imepakwa rangi.
– Cha mwalimu kimeongezeka.
– Ya mawe imenyesha.
(i)Viwakilshi vya enye, enyewe, ote, ingine (pekee).
Mfano:
– Mwneye sumu amefika.
– Chenyewe kimechacha.
– Wote wamestaafu.
– Mwingine ameonekana.
VITENZI(T),
Ni maneno ambayo hueleza jambo lililofunywa na nomino au kiwakilshi
Mfano:
– Baba analima shambani.
– Shamba letu limepandwa migomba.
– Sisi tunasoma somo la Kiswahili.
AINA ZA VITENZI
a. Kitenzi kikuu (T).
b. Kitenzi kisaidizi (TS).
c. Kitenzi kishirikishi (t).
(a) Kitenzi kikuu (T).
Ni kitenzi ambacho hueleza jambo lililofanywa na nomino au kiwakilishi. Mfano soma, lima, pika,
cheza.
Mfano:
Mtoto anacheza mpira.
Chakula kimepikwa vizuri.
Mwlaimu anafundisha darasani.
Neema anakula ugali.
Mvua imenyesha jana.(b)Kitenzi kisaidizi (TS)
Ni kitenzi ambacho hukaa sambabma na kitenzi kikuu kukisaidia kukamilisha taarifa.
Mfano:
a. Mama alikuwa nalima bustani.
b. Daima alikuwa amenunua chapati
c. Kondoo aliyepotea amepatikana.
d. Sherehe ilikuwa imeanza muda huo.
e. Sofia alikuwa amelalia tofali.
f. Kesho tutakuwa tumemaliza kazi.
Kitenzi kishirikishi (t).
Ni neno linaloonesha kuwepo kwa hali au tabia ya mtu au kitu
Mfano
a. Mti huu ni mrefu.
b. Wewe ni mwongo.
c. Mtoto wetu si mwizi.
d. Gari lake li kasi.
e. Mimi si mwoga.
f. Mashaka ndiye mpishi.
Uyakinishi Ukanushi
Juma ni mtoto. Juma si mtoto.
Chakula ni kitamu. Chakula si kitamu.
Huyu ndiye mwizi. Huyu siyo mwizi.
VIELEZI(E).
Ni maneno yanayotoa habari zaiidi kuhusu kitendo kilivyofanyika kinavyofanyika na kitakachofanyika
Mfano
o Dada anatembea polepole.
o Wavulana wamecheza uwanjani.
o Wanafunzi wanakwenda nyumbani.
AINA ZA VIELEZI.
a. Vielezi yva wakati au muda.
b. Vielezi vya mahali.
c. Vielezi vya idadi/kiasi.
d. Vielezi vya namna/jinsi.
(a)Vielelzi vya wakati au muda.
Huonyesha tendo limetendeka wakati gani.
Mfano:
– Maimuna aliamka alfajiri.
– Juma alikuja usiku.
– Ng`ombe alikuja jioni.
– Asha alifika saa moja.
– Kuku aliletwa jana.
– Mtaondoka mwezi ujao.
– Alifika hapa jua kichwani.
(b)Vielezi vya mahali.
Huonesha mahali kitendo kilipotokea.
Mfano:– Tutaonana shuleni.
– Mkutano ulifanyika kwa mkuu wa wilaya.
– Bibi anapika jikoni.
– Baba amekaa sebuleni.
– Gari linapita njiani.
– Mama alienda sokoni.
– Kaka ameenda shambani.
©vielezi vya idadi au kiasi.
Hivi hufafanua mara ngapi kitendo kinachozungumzwa kimetendeka.
Mfano:
– Tuligombana mara nyingi.
– Nilisubiri kidogo.
– Alionekana mara moja moja.
– Juma alisoma mara chache.
– Juma anaimba kila mara.
– Musa anaenda sokoni mara kwa mara.
– Debe limejaa pomoni.
(d)vielizi vya namna au jinsi.
Huonesha jinsi kitendo kinavyotendeka.
Mfano
Daudi alicheza vizuri.
Musa aliimba vibaya.
Juma amesimama wima.
Asha anasoma ovyo.
Samweli anatembea haraka haraka.
Msicheze kihuni.
(e) vielezi viulizi.
Ni vielezi ambavyo huuliza juu ya tendo lilifanyika lini, wapi na namna gani.
Mfano:
– Mwlaimu anafundisha wapi?
– Juma atarudi lini?
– Juma aliandika vipi?
(f)kielezi kiigizi
Ni kielezi ambacho huonesha jinsi tendo lilivyotendeka kama kuiga sauti au mlio unaotokana na tendo
hilo.
Mfano
– Kitambaa hicho kilichanika chaa!
– Machozi yalitiririka tirir!
– Alichapwa na kulia meee!
– Juma alianguka chini puu!
KIVUMISHI (V)
Ni neno linaloelezea sifa au linalotoa taarifa zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi.
AINA ZA VIVUMISHI.
a. Vivumishi vya kumiliki.
b. Vivumishi vya idadi.
c. Vivumishi vya sifa.
d. Vivumishi vya kuuliza.
e. Vivumishi vya kuonesha.f. Vivumishi vya majina/jina kwa jina.
g. Vivumishi vya kurejesha/amba.
h. Vivumishi vya A- unganifu.
i. Vivumishi vya enye, enyewe, ole, (pekee).
(a) Vivumishi vya kumiliki
Ni vivumishi ambavyo hutumika kuonesha umiliki wa nomino au viwakilishi.
Mfano:
– Nguo zangu zimekauka.
– Mtoto wao ni mrembo.
– Gari yangu imechafuka.
– Ng`ombe wangu wameonekana.
(b)vivumishi vya idadi.
Ni aina ya kivumishi au maneno ambayo hutaja idadi ya vitu au watu.
Mfano:
– Wanafunzi watano wamekula.
– Viti vichache vimenunuliwa.
– Mtoto mmoja ameonekana.
– Kuku wengi wamekufa.
(c)vivumishi vya sifa.
Ni maneno yanayotoa sifa mbalimbali za nomino au viwakilishi.
Mfano
Kijana mrefu amekuja.
Simba mkali ameuwawa.
Vitabu vizuri vinauzwa.
Ng`ombe mweusi amekufa.
Mtoto mwizi amekamatwa.
Kijana mfupi hajafikia tawi la mti.
Mtoto mchafu ameoga.
Dawa chungu imeletwa.
(d)vivumishi vya kuuliza.
Ni maneno yanayotumika kuuliza swali.
Mfano:
– Nyumba ipi imeuzwa?
– Nchi gani imechukua kombe?
– Watoto wapi wamefaulu?
– Nguo zipi zimechukuliwa?
(e) vivumishi vya kuonesha.
Ni maneno ambayo huonesha vitu vya karibu au mbali.
Mfano:
– Bata huyu amepikwa.
– Jembe lile limevunjika.
– Majembe yale yanakutu.
– Watoto hawa ni wazembe.
(f) vivumishi vya majina au jina kwa jina
Haya ni majina yanayotumika kueleza zaidi maana ya majina mengine.
Mfano:
– Bata mzinga aliyepotea amepatikana.
– Askari kanzu amefanikiwa kumtambua mhalifu.- Paka shume amepotelea porini.
– Ofisa mtendaji amekagua mazingira.
– Bwana afya ameonja chakula.
(g)vivumishi vya kurejesha au amba.
Mfano:
– Kiatu ambacho kinanuka.
– Jicho ambalo halioni.
– Bata ambaye ametaga.
– Mtoto ambaye amefaulu.
– Samaki ambao wameoza.
(h)vivumishi vya a- unganifu.
Haya ni maneno yanayotoa taarifa kuhusu nomino kiwakilishi kwa kuunga taarifa hiyo na nomino
kutumia maneno yanayoishia na irabu “a”.
Mfano:
Godoro la pamba limechoka.
Kiti cha mbao kimevunjika.
Kitabu cha mwalimu ni kizuri.
Gari la baba linasifiwa sana.
Jino la tembo ni mali.
Kisu cha chuma kimevunjika.
(i)vivumishi vya enye, enyewe,ingine,ote(pekee).
Vivumishi hivi huonesha umilikisho kwa mfano mtu mwenye busara ni sawasawa na mtu wa busara.
Mfano
o Mtoto mwingine amepotea.
o Mhalifu mwenyewe ametoroka.
o Kuku mwenye sumu amekufa.
o Chakula chenyewe kimechacha.
o Wazee wote wamestaafu.
o Kobe mwingine ameonekana.
o Mvulana mwenye ulemavu ameshinda.
o Amekula ubwabwa wote.
KIUNGANISHI (U)
Haya ni maneno ambyo hutumika Au
Ni maneno yanayoungnaisha maneno mengine.
Mfano:
– Baba analima na mama anapika.
– Mjomba anaenda lakini shangazi hajaenda .
AINA ZA VIUNGANISHI.
kuungaisha vipande vya lugha ili kuunda kipashio kikukubwa zaidi.
(a)Kiunganishi huru.
KUPATA NOTES KAMILI WASILIANA NASI
0675701982/0743441251/0679241251
NOTES LESSON PLAN
EXAMS
SCHOOL ACTION PLAN