February 26, 2026

WatuCrash

📚 Education & Learning Hub (Primary + Secondary)

Social Studies

NUKUU ZA MAARIFA YA JAMII DARASA LA SITA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA

TEKNOLOJIA

NUKUU ZA SOMO

(ZILIZORAHISISHWA)

MAARIFA YA JAMII

DARASA LA VISURA 1: MAJANGA YATOKANAYO NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

1.1 Dhana ya Mabadiliko ya Tabianchi

Tabianchi ni wastani wa hali ya hewa ya eneo fulani iliyorekodiwa kwa kipindi cha muda mrefu kawaida ni miaka

30 au zaidi.

Mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko makubwa ya wastani ya hali ya hewa inayorekodiwa kwa kipindi cha muda

mrefu kawaida ni miaka 30 au zaidi. Mabadiliko ya tabianchi hutokea pale ambapo mabadiliko ya mfumo wa

kawaida wa tabia yanayosababishwa mwenendo mpya wa hali ya hewa duniani kwa miongo au karne nyingi.

Mabadiliko ya tabianchi pia husababishwa zaidi na ongezeko la joto duniani.

Umuhimu wa Kujua Tabianchi ya Tanzania

(a). Kufahamu tabianchi hutuusaidia kubainisha mwenendo wa muda mrefu wa vipengele vya hali ya hewa kama

vile mvua, jotoridi, mgandamizo wa hewa, unyevuanga, nuru ya jua, mawingu na upepo.

(b). Tabianchi hutuuwezesha kupanga shughuli za kiuchumi na kijamii zinazoweza kufanyika katika eneo

fulani mfano: kilimo cha chai kwenye mvua nyingi, ufugaji kwenye sehemu zenye nyasi fupi.

(c). Ufahamu juu ya tabianchi hutusaidia kupanga aina ya nguo za kuvaa, au namna ya kujenga nyumba

ya kuishi.

Mambo yanayoathiri tabianchi ya eneo fulani

(a). Latitudo ya eneo; ni umbali kutoka mstari wa ikweta. Maeneo yaliyo karibu na mstari wa ikweta hupokea kiasi

kikubwa cha nuru ya jua kuliko maeneo yaliyo mbali na ikweta. Hivyo, maeneo haya huwa na joto jingi kuliko

maeneo yaliyo mbali na ikweta.

(b). Mwinuko kutoka usawa wa bahari; maeneo yenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa

ya Kilimanjaro, Iringa, Njombe na Arusha huwa na baridi na mvua nyingi. Kadri mwinuko kutoka usawa wa

bahari unayvoongezeka, jotoridi hupungua kwa wastani wa nyuzi 0.60C kwa kila meta 100.

(c). Sura ya nchi; ni umbile la eneo fulani kama vile milima na mabonde. Sehemu zenye milima huathiri mienendo

ya upepo na mvua. Upande wa mashariki mwa milima hupata upepo wenye unyevu mwingi kutoka baharini

ambayo hufanya mawingu na kuleta mvua. Upande wa magharibi hupata upepo usio na unyevu hivyo kupata

mvua kidogo au kukosa mvua kabisa.

1.2 Ongezeko la joto duniani

Ongezeko la joto duniani ni hali ya kuongezeka kwa taratibu lakini kwa uhakika kwa wastani wa joto katika uso wa

duniani. Ongezeko hili linasababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha gesijoto angani. Gesijoto hizi ni kama vile

hewa ya ukaa/kabonidayoksaidi, mvuke, methani na ozoni. Ongezeko la joto duniani hubainika kwa kulinganisha

vipimo vya joto vinavyopatikana katika nyakati tofauti.

1.3 Uhusiano kati ya shughuli za kibinadamu na ongezeko la joto duniani

Uhusiano kati ya ongezeko la joto duniani na shughuli za kibinadamu huonekana katika uzalishaji wa gesijoto.

Shughuli mbalimbali za kibinadamu zimekuwa zikichangia uzalishaji wa gesi hususani hewa ya

ukaa/kabonidayoksaidi. Nguvu za kiasili kama vile mlipuko wa volcano zimechangia pia katika uzalishaji wa

gesijoto.

Gesi hizi zinapozalishwa hupaa angani na kutengeneza utando mzito mfano wa blanketi. Utando huu huzuia baadhi

ya miale ya jua iliyoakisiwa kwenye uso wa duni kupenya na kusafiri anga la nje. Hivyo, joto hili hurudi duniani na

kusababisha ongezeko kubwa la joto. Baadhi ya shughuli za kibinadamu zinazochangia ongezeko la joto duniani ni

kama vile: ukataji wa miti na matumizi ya fueli za kisukuku. Ukataji miti

Uoto wa asili unafaida nyingi katika mazingira kama ifuatavyo: hupunguza kiwango cha mwanga wa jua

kinachoakisiwa na kurudishwa kwenye uso wa dunia na hivyo kupunguza joto duniani; hupunguza hewa ya

kabonidayoksaidi katika angahewa pale inapojitengenezea chakula chakula chake.1.4

1.5 Miti inapokatwa huongeza gesijoto ya kabonidayoksaidi angani hivyo kuchangia ongezeko la joto duniani. Miti hii

hukatwa kwa ajili ya makazi na kilimo.

Matumizi ya Fueli za Kisukuku

Nishati ya fueli za kisukuku hutumika kwenye sekta ya viwanda, umeme, usafirishaji na ujenzi, licha ya kuwepo

nishati mbadala kama jua na upepo. Hata hivyo matumizi ya fueli hii huchangia ongezeko la joto duniani kutokana

na uzalishaji wa gesijoto kwa kiasi kikubwa na hatimaye mabadiliko ya tabianchi.

Uhusiano kati ya ongezeko la joto duniani na majanga

Uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za binadamu kumesababisha ongezeko la joto duniani na hatimaye

mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha kutokea au kuongezeka kwa madhara ya majanga

ambayo yanaathiri shughuli za kila siku za binadamu na miundombinu. Dhana ya Majanga

Majanga ni matukio ya ghafla katika jamii zetu yanayotokea bila taarifa. Majanga yanaweza

kusababishwa na nguvu za kiasili au shughuli za kibinadamu. Majanga yanayosababishwa na nguvu za

kiasili ni kama vile ukame, tetemeko la ardhi, mafuriko, vimbunga, milipuko ya volkano na maporomoko

ya udongo.

Baadhi ya majanga yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu ni kama vile ajali (za barabarani, majini,

angani, viwandani, reli) moto unaotokea nyumbani na msituni. Vile vile utupaji wa taka ovyo na ujenzi

holela husababisha mikondo na mitaro ya maji kuziba hatimaye mafuriko wakati wa mvua. Baadhi ya

athari zinazosababishwa na majanga haya ni kama vile, ukame unaoweza kusababisha upungufu au

kukosekana chakula cha mifugo cha mifugo na binadamu hali inayosababisha vifo. Pia, husababisha

uharibifu wa mali kama miundombinu, mazao na mifugo.

Athari za kuongezeka kwa joto duniani

Ongezeko la joto duniani limesababisha mabadiliko ya tabianchi kwa sehemu nyingi duniani. Ongezeko la joto

limekuwa na athari zifuatazo:

(a). Kutokea mara kwa mara kwa manjanga yanayohusiana na hali ya hewa na tabianchi kama vile ukame na

mafuriko.

(b). Kutokea mara kwa mara matukio ya hali ya vimbunga na upepo mkali.

(c). Kuharibiwa na kupungua kwa kiwango cha theluji katika milima mirefu na maeneo yenye barafu.

(d). Kuongezeka kwa mvua kubwa ndani ya kipindi kifupi na kusababisha mafuriko. Kuongezeka kwa joto

duniani huongeza joto la bahari na kusababisha uvukizwaji mkubwa angani unaoleta mawingu na

kusababisha mvua kubwa ziletazo mafuriko.

(e). Kuyeyuka kwa barafu na theluji kutoka ncha za dunia na hivyo kuongeza ujazo wa maji baharini na

kuhatarisha makazi ya watu wanaoishi karibu na bahari au visiwani.1.6 Majanga yasababishwayo na ongezeko la joto duniani

(a) Ukame

Ukame ni hali ya ukosefu wa mvua zinazotegemewa katika eneo fulani kwa muda mrefu. Wakati wa ukame mvua

hunyesha chini ya kiwango cha wastani kwa eneo husika.Ukame unapotokea huambatana na ukosefu wa maji,

chakula na malisho kwa ajili ya watu na mifugo. Wakati wa ukame kunakuwa na joto kali wakati wa mchana na

baridi wakati wa usiku vikiambatana na upepo mkali.

Tofauti kati ya Kiangazi na Ukame: Kiangazi ni majira ya mwaka yanayobainishwa na ukosefu au uwepo wa

mvua kidogo. Kiangazi hutokea kila mwaka, na hivyo sio janga kama ilivyo ukame.

Uhusiano kati ya mabadiliko ya tabianchi na ukame; kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ukame hutokea mara

nyingi zaidi na hudumu kwa muda mrefu zaidi.

Kwa hapa Tanzania ukame huathiri zaidi mikoa ya kanda ya kati na kaskazini: Dodoma, Arusha, Manyara, Singida,

Shinyanga, Simiyu na Kilimanjaro.

(i) Athari za Ukame

Baadhi ya madhara ya ukame ni kama yafuatayo:

(a). Vifo vya watu, mifugo, na mimea kutokana na ukosefu wa chakula na maji.

(b). Kukauka kwa mazao shambani na hivyo kusababisha upungufu wa chakula.

(c). Kupungua kwa mapato yanayotokana na kilimo na mifugo kwa wakulima na serikali. Hali hii hutokana na

kufa kwa mifugo na kukosekana kwa mavuno.

(d). Ukame husababisha kutokea kwa mmomonyoko wa udongo kutokana na upepo na kuharibika kwa tabaka la

juu la udongo.

(e). Kukauka kwa vyanzo vya maji kama vile mito, mabwawa, visima, au vijito na kupungua kwa kina cha maji

kwenye maziwa na mabwawa makubwa.

(f). Ukosefu wa nishati ya umeme utokanao na maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji kwenye mabwawa.

(g). Kuhama kwa wanyamapori kutoka mbugani hadi kwenye makazi ya watu wakitafuta maji ya kutosha na

malisho.

(h). Kuongezeka kwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na ukosefu wa maji na malisho ya mifugo.

(i). Kutokea na kuongezeka kwa moto katika misitu na kutishia maisha ya wanyama na watu.

(ii) Mbinu za kukabiliana na athari za ukame

(a). Kupanda mazao yanayostahimil ukame na kukomaa kwa muda mfupi mfano mtama, uwele na mihogo.

(b). Kuhimiza uendeshaji wa kilimo hifadhi ili kupunguza upotevu wa maji na kuhifadhi rutuba ya udongo.

(c). Kuhimiza kilimo cha umwagiliaji.

(d). Kutoa elimu kwa jamii kuhusu kilimo hifadhi, kilimo cha umwagiliaji, aina nzuri za mbegu za mazao na

matumizi bora ya pembejeo.

(e). Kuhimiza ufugaji bora na wa kisasa unaozingatia mifugo michache inayohimili mazingira ya ukame.

(f). Mamlaka ya hali ya hewa kuwa na mfumo imara wa tahadhari ya mapema kwa wadau kuhusu mwenendo wa

mvua.

(g). Kuwa na mipango ya kukabiliana na majanga.

(b) Mafuriko

Mafuriko ni janga ka kiasili ambapo eneo ambalo kwa kawaida huwa nchi kavu hufunikwa na maji mengi kwa

ghafla. Mafuriko ni janga ambalo linaweza kuleta madhara makubwa. Zipo sababu mbalimbali zinaposababisha

kutokea kwa mafuriko.Sababu za kutokea kwa mafuriko

(a). Kunyesha mvua nyingi katika kipindi kifupi au kipindi kirefu.

(b). Kuzidiwa kwa mito, vijito, mabwawa, maziwa na bahari kunakolazimisha maji kutofuata uelekeo wake. Hali

hii husababisha maji kuelekea kwenye sehemu zisizotakiwa kama vile makazi, shambani, viwandani.

(c). Kupasuka kwa mabwawa makubwa yanayotumika kuhifadhia maji kwa ajili ya kuzalisha umeme au

umwagiliaji.

(d). Kuyeyuka kwa barafu au theluji katika ncha za kaskazini na kusini mwa dunia, kutokana na kuongezeka kwa

joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

(e). Ongezeko la joto duniani husababisha kuongezeka kwa joto la bahari. Hali hii kuongeza uvukizwaji mkubwa

angani na kuleta vimbunga kwenye maeneo ya fukwe za bahari. Hii husababisha mafuriko kwenye maeneo ya

pwani.

(f). Kuziba kwa mirefereji ya maji kwenye makazi yetu kunakosababishwa na uchafuzi wa mazingira hususani

utupaji ovyo wa taka ngumu. Taka hizi huziba mifereji hivyo maji kukosa mahali pa kutiririkana hivyo

KUPATA NOTES KAMILI WASILIANA NASI

0675701982/0743441251/0679241251

 NOTES

 LESSON PLAN

 EXAMS

 SCHOOL ACTION PLAN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *