NUKUU ZA SOMO LA KISWAHILI 2025 DARASA LA NNE
ZABIKHA ISLAMIC NURSERY AND PRIMARY SCHOOL
NUKUU ZA SOMO LA KISWAHILI 2025 DARASA LA NNE
11.0 KUWASILIANA KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI
1.1 Kuendeleza mazungumzo katka miktadha mbalimbali.
a) Kulinganisha vitu kwa kutumia maneno [kuliko,Zaidi ya ,kama mithili
ya na mfano wa] katika miktadha mbalimbali
i. Kujenga dhana ya ulinganishi
Ulinganishi ni hali ya kuwa sawa
Ukubwa na udogo wa kitu ni mwonekano wake unaotokana na
umbo lake au eneo lake.
– Kutaja majina ya vitu mbalimbali vinavyopatikana katika
mazingira;Kiti,meza,kitanda,sahani,kijiko,upawa,mwiko,milima,
magari,
Magari,pikipiki, tikiti,dirisha,simu,mnazi,gauni,nyumba,ghorofa
na kitana.
ii. Kulinganisha vitu mbalimbali kwa kutumia maneno [kuliko,Zaidi
ya,kama mithili ya na mfano wa]
Ifuatayo ni mifano mingine ya ulinganishi:
1. Kiatu kile ni kikubwa Zaidi ya hiki
2. Chumba change ni kikubwa kuliko
3. Mlango ule ni mkubwa Zaidi ya huu
4. Dada yangu ni mdogo kuliko dada yako
5. Shamba hilini dogo kuliko lile
6. Kalamu hii ni ndogo Zaidi ya ile
7. Kitabu chetu ni kidogo kuliko kitabu chao
8. Upana wa shule yetu ni kama wa shule yenu
9. Ukubwa wa Dar es Salam si sawa na wa Dodoma
10. Rangi ya viatu si sawa na rangi ya viatu vyangu
2Tunatumia maneno kama vile kama na sawa na kulinganisha
Ukubwa na Udogo wa vitu vinavyofanana.
Mfano:
1. Mtoto huyu ni mdogo kama sungura
2. Ukubwa wa gari lao ni sawa na wa gari letu
3. Shamba langu ni dogo kama lile la mjomba
4. Shangazi yangu ni mrefu kama mjomba
5. Unene wa kiatu hiki ni sawa na wa kile pale
Zoezi 1
Jibu maswali yafuatayo sahihi
1. Andika kweli kwa kauli ambayo ni sahihi na Si kweli kwa
kauli ambayo si sahihi
a) Mji wa Zubeda ni mdogo kuliko wa Sara
b) Mji wa Sara una barabara chache kuliko mji wa
Zubeda
c) Miji yote miwili ina idadi sawa ya watu
d) Sara alitembelewa na Zubeda
2. Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo
ya ulunganishi:
a) Kama
b) Sawa na
c) Kuliko
d) Zaidi ya
e) Mithili
32. kutumia miundo Chora picha za michoro ifuatayo kisha linganisha kwa
( Sawa na ,kuliko, kama na Zaidi ya )
a. Kikombe
b. Gauni
c. Chupa
d. .Dirisha
b ) Kusimulia matukio kwa kuzingatia njeo za wakati ; uliopo[-na-
],uliopita[-li-],ujao ta,[- -],mazoea,[-hu-] na hali timilifu [-me-]
i. Kueleza matukio kwa kutumia nyakati mbalimbali katika
sentensi.
– Kutaja nyakati mbalimbali za utendaji
Wakati ni nini?
Wakati ni muda unaoashiria tendo au tukio Fulani lililofanyika au
linavyofanyika na litakavyofanyika.
– Nyakati zimegawanyika katika sehemu kuu tano
a. Wakati uliopita [LI]
b. Wakati uliopo [NA]
c. Wakati ujao [ TA]
d. Wakati mtimilifu [ ME]
e. Wakati wa mazoea [HU]
i. Kueleza matukio mbalimbali kwa kutumia nyakati anazojifunza
4Wakati uliopo [NA]
Wakati uliopo ni muda unaoashiria kuwa tendo linaendelea
kutendeka.
Mfano;
1. Wanafunzi wanasoma darasani
2. Sisi tunalima bustani
3. Nyinyi mnaoga bafuni
4. Wageni wanaingia ndani
5. Yeye anaimba taratibu
6. Unakula ugali na kitoweo gani?
7. Mjomba anapalilia shamba
8. Mnatembeataratibu sana
9. Wao wanapigana ngumi
10. Mama anaswali asubuhi
Wakati ujao [TA]
Wakati ujao ni muda unaoashiria kuwa tendo litafanyika badae.
Mfano;
1. Wanafunzi watafunga shule mwezi ujao
2. Walimu wataandika kitabu kizima
3. Sisi tutakula chakula kizuri
4. Watapalilia shamba lao
5. Yeye hataondoka mpaka amalize kazi
6. Mtakimbia wapi?
7. Yeye ataswali adhuhuri
8. Sisi tutampiga hadi afe
9. Tutaandika kama tulivyoelekezwa
5Wakati uliopita [LI]
Wakati uliopita ni muda unaoashiria kuwa jambo /tendo lilitendeka muda
mrefu uliopita
Mfano;
1. Alinunua debe la senene jana
2. Mgonjwa alipelekwa hospitali
3. Tulikula wali na tulikunywa maji
4. Walichimba kisima kirefu
5. Wao waliimba wimbo mzuri
6. Muliingia ukumbini saa ngapi?
7. Mwalimu aliingia darasani
8. Mwanafunzi aliandika somo
9. Mimi nilisoma kitabu cha kiswahili
Wakati mtimilifu [ME]
Wakati mtimilifu ni wakati unaoashiria tendo limefanyika punde tu [sio
muda mrefu]
Mfano;
1. Ameondoka leo asubuhi
2. Wameingia madarasani
3. Amekula chakula chote
4. Tumesoma dua leo asubuhi
5. Wao wamebeba madawati
6. Mwalimu amewaadhibu wanafunzi wakorofi
7. Wale wmegombana
8. Asha amejifungua leo asubuhi
69. Sisi tumekunywa kahawa
Zoezi 1
Andika sentensi hizi katika wakati mtimilifu
1. Wanafunzi walifanya mgomo
2. Baba ataezeka nyumba
3. Daktari analing`oa jino
4. Nitaandika waraka mpya kwa baba yangu
5. Wale wamegombana
Andika sentensi katika uliopo
1. Vyura hao waliishi kwenye miji miwili
2. Walisalimiana katika safari
3. Mji wa kaskazini ulikuwa mbali na wa kusini
4. Baba alirudi jana jioni
5. Wote walipanda juu
Wakati wa mazoea [ HU]
Wakati wa mazoea ni wakati unaoanesha huwa kkitendo hufanyika kila
siku na mara kwa mara kitendo hicho hufanyika.
Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa usahihi
Sifa za mbweha
Mbweha nu mnyama mdogo wa porini anayefanana na mbwa. Ana
mdomo uliochongoka ,maskio yaliyosimama na mkia weny manyoya
mengi.
Mbweha huishi kwenye vichaka .Mnyama huyu huwinda na kutafuta
chakula chake usiku. Maana yake ni kuwa mbweha hulala wakati wa
mchana . Anapowinda , hurukia mawindo yake kama wafanyavyo
7paka.Mbweha hula wanyama kama vile sungura,mijusi na panya .Vilevile
,hula wadudu mbalimbali na hata matunda.Mnyama huyu huweza
kupanda hata juu ya miti..
Mbweha huzaa mara moja kwa mwaka huweza kuzaa watoto hadi
kumi .Mbweha anapozaa ,Jike hukaa na watoto na dume huenda
kuwinda na kuleta chakula .Masikio ya mbweha husikia panya wakiwa
wanachimba chini aridhini.
Hakika yapo mambo mengi ya kuvutia yanayomhusu mnyama huyu
mbweha.
Zoezi 2
Badili sentensi zifuatazo kuwa katika hali mazoea
1. Mimi numepiga mswaki asubuhi
2. Sisi tunacheza mpira jioni
3. Nyinyi mnaenda kulima
4. Yule amesoma vitabu vya hadithi
5. Wao wamefaulu somo la hisabati
6. Nuru na Chitola wamefanya maigizo
Zoezi la 3
Chagua neno sahihi kwenye kisanduku ili kukamilisha sentensi.
Akajichubua,nguzo,mabuyu,matunda,kivuli,madawati
1. Matunda ya mbuyu yanaitwa _______________
2. Wakati wa jua kali tunakaa kwenye ___________
83. Nyumba nyingi kijijini zimejengwa kwa __________
4. Maji ya ___________ ni matamu sana
5. Wanafunzi darasani wanakalia ____________
6. Alijikwaruza kwa jiwe _______________ ngozi yake
iii. Kukanusha matukio ya nyakati mbalimbali kwa kutumia sentensi.
a) Kueleza maana ya ukanushi
Ukanushi ni nini ?
Ukanushi ni tendo la kupinga au kukataa jambo Fulani .
Tunapokanusha sentensi tunadondosha baadhi ya silabi katika kitenzi au
tunabadili na kuongeza baadhi ya silsbi lakini hatubadili maana ya msingi
ya neno.
Mfano : 1
KUPATA NOTES KAMILI WASILIANA NASI
0675701982/0743441251/0679241251
 NOTES
 LESSON PLAN
 EXAMS
 SCHOOL ACTION PLAN
9