January 13, 2026

WatuCrash

📚 Education & Learning Hub (Primary + Secondary)

ca-app-pub-5779332594648854/1423561520
Civic and Moral Education

NUKUU ZA URAI NA MAADILI

NUKUU ZA URAIA NA 

MAADILI DARASA LA SABA 

KUHESHIMU JAMII 

1.1 Kujipenda na kuwapenda wengine 

i. Katika mada hii tutajifunza dhana ya familia. ii. Jinsi ya kupenda jamii zetu katika familia. iii. Ni jinsi gani ya kusaidia familia zenye mahitaji na ambazo zina mahitaji maalumu. iv. Jinsi gani ya kuthamini familia zetu na kuziheshimu. 

v. Kushirikiana na jamii familia katika kutekeleza haki za jamii zinapatikana na zinaheshimiwa. 

vi. Kuwaheshimu wanajamii na kuwapenda hasa kutokuwepo ubaguzi wa aina yoyote ili kila mwanajamii aweze kupata upendo, heshima na uhuru wake. 

Fikiri: 

Kuna faida zipi tunapowapenda wenzetu katika jamii 

– Kutakuwepo na amani, upendo na mshikamano 

– Ubaguzi hautakuwepo 

– Heshima itajengeka katika jamii 

– Kila mtu ambaye ni mwanajamii atakuwa huru na ataona thamani ya kuwepo kama mwanajamii katika kuelimisha kutoa msaada na kujali wenzetu. 

Mada ndogo 

Kuelimisha jamii namna ya kutoa msaada kwa wahitaji: 

Wahitaji: 

Ni watu waliopungukiwa na mahitaji muhimu katika jamii. 

Mahitaji hayo ni kama vile: 

a) Chakula 

b) Mavazi 

c) Malazi 

d) Fedha na n.k 

– Tunatakiwa kuelimisha jamii na kuhamasisha jamii itoe misaada na izingatie hasa wahitaji katika jamii kwa kufuata yafuatayo ambayo ni:-

a) Kubaini makundi yenye mahitaji maalumu katika jamii. 

b) Kufahamu kila kundi linahitaji msaada wa namna gani. 

c) Kujua njia za kuhamasisha na kuelimisha jinsi ya kutoa misaada kwa makundi ya wahitaji. 

d) Kujua jinsi ya kuwafariji wahitaji katika jamii. 

e) Kungalia huduma na faraja tunazoweza kuwapatia wahitaji katika jamii zetu. 

f) Kufahamu umuhimu wa wahitaji katika jamii zetu. 

g) Kupanga mikakati ya kuwatambua wenye uhitaji katika jamii na makundi yanayofaa kuwasaidiwa. 

a) Makundi muhimu ya wahitaji katika jamii. 

Wahitaji ni nini katika jamii? 

Wahitaji ni jumla ya makundi ya watu mbalimbali katika jamii wenye mahitaji muhimu kuliko wanajamii wengine. 

Wahitaji hao wako katika makundi kama yafuatayo: 

i. Watu wenye ulemavu mfano walemavu wa viungo, albino, walemavu wa macho n.k ii. Wazee mfano wasiojiweza katika kufanya kazi za kuwaingizia vipato 

iii. Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mfano kama watoto yatima au wanaozunguka mitaani 

iv. Waathirika wa majanga mbalimbali kama vile; mlipuko wa magonjwa, mafuriko, janga la njaa, tetemeko la ardhi na vita. 

Watu wakipata misaada mbalimbali-picha 

Utoaji wa misaada kwa waathirika wa mafuriko-picha 

Zoezi 

1. Watu wanaopungikiwa na mahitaji katika jamii zao huitwaje? 

Jibu: Huitwa wahitaji 

2. Taja makundi ya watu wenye uhitaji katika jamii: 

Jibu: makundi hayo ni: 

Walemavu, wazee, watu waliopatwa na mafuriko, watu wenye mlipuko wa magonjwa, wenye kupatwa na majanga ya moto, wajane na wazee. 

3. Ni faida gani wanayopata wahitaji katika jamii. 

Jibu: 

b) Jamii inawathamini na kuwapenda 

c) Jamii inalinda haki zao za msingi kama haki za binadamu ili zisivunjwe juu yao 

d) Kupata misaada mbalimbali kwa kupitia jamii, mashirika binafsi, pamoja na serikali 

e) Kupatiwa elimu juu ya matatizo waliyonayo ili wajilinde 

4. Ni jinsi gani unavyoweza kumsaidia mwanafunzi mwenye uhitaji: 

Jibu: 

i. Nitamuhoji nijue tatizo alilo nalo na kujua ni hitaji gani hasa muhimu analohitaji 

ii. Nitamshauri ajione kuwa naye ni mtu wa muhimu sana katika jamii ili ajenge kujiamini na kujithamini. iii. Nitampatia mahitaji mfano penseli, peni, rula daftari na ufutio. 

iv. Nitaongozane naye kwa mwalimu mkuu ili ahojiane naye kama kuna nguo za shule za misaada apewe. 

v. Nitamshauri asome kwa bidi ili afaulu mitihani yake vizuri 

vi. Kama mwanafunzi ni mlemavu nitamsaidia mfano kumshika mkono kumpeleka chooni, kumpeleka kucheza na kumrudisha nyumbani. vii. Nitampatia nguo za kuvaa kwa kushirikiana na wazazi wangu wamnunulie. 

viii. Nitakula na yeye chakula ambacho nitakuwanimepewa ni shuleni. 

Aina za misaada kwa wahitaji: 

Ipo misaada ya aina nyingi ambayo inatakiwa kutolewa kwa wahitaji misaada hiyo ni kama:-

Chakula, malazi, mavazi, usafiri, fedha, huduma za afya, vifaa vya kutumia mfano kwa walemavu kama baiskeli, magongo ya kutembelea kuwapa ushauri bora pamoja na kuwapa malezi bora, upendo na kuwathamini. 

Misaada kama hii ya uhitaji hutolewa katika jamii zetu pale kunapotokea matatizo mbalimbali, mfano kama mlipuko wa magonjwa, watu ufariki na kuacha watoto yatima ambao huhitaji msaada kama wa kupelekwa shule, hivyo huhitaji vifaa kama sare za shule, madaftari, pamoja na viatu, soksi, na peni hivyo wanajamii hutoa huduma. Pia kama swala la mafuriko mfano jangwani, mto msimbazi na mafuriko ya huko mkoani Mtwara, mafuriko haya yamesababisha matatizo makubwa katika jamii na wahitaji kuwa wengi, wahitaji hawa huitaji chakula, mavazi, malazi na makazi ya kuishi, hivyo kusababisha jamii ichange nguo, fedha, chakula ili kuwapatia waweze kuishi. Pia wahitaji hawa wanaweza kupatiwa ushairi na unasihi ili waweze kuhimili changamoto wanazokutana nazo shuleni, nyumbani na katika mazingira yoyote watakapokuwa. Wahitaji hawa pia huitaji huduma za afya ili wapatiwe dawa endapo mfano kuna magonjwa kama ugonjwa wa CORONA, kipindupindu, n.k. wahitaji hawa wanaitaji elimu bora kwa mfano kupelekwa shuleni ili waweze kujikwamua wenyewe endapo watafaulu na kupata kazi. Pia wahitaj hawa huhitaji ushauri wa kisheria kwa ajili ya kuwatetea endapo kuna matatizo huitaji wataalamu waliobobea mambo ya sheria ili kuweza kuwatetea na kupata haki zao mfano kama wamedhulumiwa ili vyombo vya haki vifuate na wapate haki zao. 

Zoezi: 

1. Ni wakati gani mwanafunzi katika kusoma kwake anaweza kuonyesha hali ya huitaji? 

Jibu: 

Mwanafunzi anaweza kuonyesha hali ya uhitaji pale anapoona masomo yameanza kuwa magumu mfano; kutoka darasa la tatu kuingia darasa la nne. Vilevile wakati wa mazoezi majaribio, mitihani ya mwisho wa mwezi na mwisho wa mwaka. Mwanafunzi huitaji msaada zaidi kwa mwanafunzi mwenzake au mwalimu wake ili aweze kufanya vizuri katika shule. 

2. Elezea baadhi ya makundi tofauti ya wahitaji: 

Jibu: Baadhi makundi tofauti ya wahitaji ni: 

a) Wazee: 

Ni watu wenye uhitaji ambao, wanahitaji kusaidiwa kama kuwafulia, kuwapikia, na kuwasaidia katika shughuli mbalimbali ambazo wao ni ngumu kuzifanya. Shughuli hizo zinaweza zikawa za kiuchumi, biashara, kisiasa na kijamii hivyo wao hawawezi kuzifanya. 

b) Wagonjwa: 

Wagonjwa ni watu muhimu ambao wanahitaji msaada mkubwa mfano wenye ugonjwa wa kansa, UKIMWI, presha, Corona na kisukari, haya ni magonjwa makubwa ambayo yanahitaji misaada kutoka kwa jamii, mashirika binafsi na serikali. Hivyo ni muhimu kuhudumia kundi hili katika jamii kwa ajili ya kulinda ushirikiano amani upendo na kutimiza haki za binadamu. c) Wahanga: 

Kuna baadhi ya majanga ambayo yanajitokeza katika nchi mfano, majanga ya mafuriko, vita, mlipuko wa magonjwa, kundi hili linahitaji mahitaji maalumu toka kwenye jamii mashirika binafsii na serikali. 

3. Msaada wa sheria unawalindaje wahitaji? 

Jibu: 

Msaada wa kisheria ni muhimu sana kwa wahitaji. Kwani unasaidia kulinda haki zao za msingi zitendeke au kutofanyika; mfano kwa watoto yatima kudhulumiwa mali zao, hivyo sheria lazima ifuatilie na kushirikiana nao wapate haki zao za msingi katika mahakama au katika sehemu husika. 

4. Taja baadhi ya njia unazoweza kuzitumia katika jamii ili kuhamasisha jamii watoe misaada kwa wahitaji: 

Jibu: 

a. Kwa kutumia njia ya vyombo vya habari kuhamasisha wananchi 

b. Kuwa kutumia mabango na vipeperushi ili wananchi wavisome na kuhamasisha jamii watoe misaaada kwa wahitaji 

c. Kwa kutumia mitandao ya kijamii. Pia unaweza kuhamasisha jamii watoe misaada kwa wahitaji. 

5. Taja baadhi ya njia unazoweza kuzitumia katika jamii ili kuhamasisha jamii watoe misaada kwa wahitaji: 

Jibu: 

a. Kwa kutumia njia ya vyombo vya habari kuhamasisha wananchi 

b. Kuwa kutumia mabango na vipeperushi ili wananchi wavisome na kuhamasisha jamii watoe misaaada kwa wahitaji 

c. Kwa kutumia mitandao ya kijamii. Pia unaweza kuhamasisha jamii watoe misaada kwa wahitaji. 

Njia za kuhamasisha jamii kutoa misaada kwa wahitaji: 

Watu kwa kushirikiana na taasisi nyingine katika jamii, hufanya jitihada mbalimbali ili kuhamasisha wanajamii kutoa misaada kwa wahitaji mbalimbali. Hizi ni njia zinazotumika ili wahitaji wapate misaada. 

a. Kwa kutumia vyombo vya habari: 

Mfano kama redio, televisheni, na magazeti hivi vinaweza kufikisha taarifa au ujumbe kwa watu wengi na kila mtu akapata taarifa. 

Mfano kwenye gazeti watu wanaweza wakasoma gazeti na kuamua kutoa msaada kwa wahitaji kupitia njia ya gazeti. Pia kwa njia ya televisheni, watu wanaweza wakaona moja kwa moja kwenye televisheni na wakawiwa hapo hapo kutoa msaada kwa wahitaji na pia kuhamasisha jamii ili ione umuhimu wa kusaidia wahitaji mfano kama (Oisi Femu) anavyohimiza na anavyoshughulikia watu wenye matatizo katika jamii (wahitaji) wapate msaada kwa kupitia vyombo vya habari. Hivyo redio na televisheni huweza kusaidia kuibua wahitaji wengi katika jamii zetu. 

b. Mabango na vipeperushi: 

Hii ni njia ambayo inaweza kutumika katika matangazo mbalimbali jamii ikasoma mabango hayo na vipeperushi na kujua wahitaji na kuwatambua ili jamii iweze kuwasaidia. Pia njia hii hudumu kwa muda mrefu sana na jamii huweza kuhamasika kuwasaidia wahitaji.  

c. Mikutano ya hadhara na semina: 

Viongozi wa dini na taasisi hutumia njia hii kutoa maelezo na hamasa kwa wananchi na jumuiya zinazowazunguka ili kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwasaidia wahitaji. 

d. Kutumia mitandao ya kijamii: 

Hii njia inasaidia jamii kupata mawasiliano haraka kwa kundi kubwa la watu kwa kupeana taarifa. 

Kwa kutumia mitandao ya kijamii wahitaji wanaweza kupata michango mingi kutoka katika jamii kwa kutoa misaada ya hali na mali. Baadhi ya mitandao ya kijamii ni kama Whatsapp, Instagram, Twitter, na Facebook. Mitandao hii ya kijamii inatumika kuhamasisha watu wengi kwa sababu makundi mengi yanatumia mitandao hiyo, kwa kutumia njia hii wahitaji wanaweza kupata misaada mingi kutoka kwa watu mbalimbali. 

e. Kutembelea nyumba kwa nyumba: 

Njia hii ya kutembea nyumba kwa nyumba hutumiwa na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu katika kusaidia wanajamii kutambua haki zao. Lengo la kutembea nyumba kwa nyumba huweza kuwa na mafanikio ya kutambua wahitaji, kuomba misaada ya wahitaji na kugawa misaada kwa wahitaji hivyo kutembea nyumba kwa nyumba kuna faida kubwa. 

Zoezi: 

1. Vyombo vya habari vinawezaje kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwasaidia watu wenye 

uhitaji? 

Jibu: 

Vyombo vya habari vinaweza kuelimisha jamii kuhusu watu wenye uhitaji kwa kufanya yafuatayo:-

– Vyombo vya habari vinaweza kutoa matangazo kwenye televisheni, kwenye redio, kwenye matangazo ya mabango, kwenye mitandao ya kijamii kama Whatsapp, facebook, twitter, na Instagram. Vyombo vya habari kwa kutumia njia hiyo ni rahisi jamii kuelimika na kusaidia watu wenye uhitaji. Pia vyombo hivyo ni rahisi kutembelea jamii na kubaini changamoto zilizopo ili kuwafanyia utaratibu wa kuomba misaada ya kuweza kuwasaidia. 

2. Eleza njia mojawapo ambayo vyombo vya habari vinaweza kutumia ili kila mwanajamii akapata taarifa juu ya watu wenye uhitaji? 

Jibu: 

Vyombo vya habari vinaweza kutumia njia ya redio. 

Njia ya redio ni njia nzuri ambayo vyombo vya habari hutumia kutoa matangazo ya mambo mbalimbali yanayohusu jamii, serikali, na dunia nzima. Chombo kama redio ni njia ambayo inafikisha taarifa kwa watu wengi wa mjini na vijijini na hivyo kila atakayesikia tangazo ni rahisi kumtangazia mwenzake. Hivyo vyombo vya habari vinaweza kuelimisha jamii kuhusu wahitaji na kila mtu akapata taarifa. 

3. Taja baadhi ya misaada ambayo inaweza kutolewa katika jamii pia ikaweza kuwasaidia wahitaji na wasiohitaji. 

a. Msaada wa ujenzi wa Barabara 

b. Misaada ya kuletewa umeme katika mitaa 

c. Ujengaji wa visima vya maji katika jamii 

d. Msaada wa kujengewa kituo cha afya (zahanati) katika mtaa 

e. Msaada wa kujengewa shule katika jamii 

4. Somo la maarifa ya jamii linafundishwa mashuleni kwa sababu gani? 

Somo la M/jamii ni somo ambalo linahusika na malezi, makuzi na maendeleo ya ukuaji wa mtu katika jamii inayomzunguka. Somo hili linasaidia sana kwani linahusu katika ujenzi wa tabia ya mtu, maadili ya nchi na maendeleo ya Taifa kiumjmla. Somo hilii linafundisha na kurekebisha mambo mbalimbali yanayoweza kuleta migogoro, matatizo na kutoweka kwa amani kati ya mtu na mtu au nchi na nchi. Vilevile somo hili linalenga kulinda haki za binadamu na kulinda rasilimali za nchi na mipaka yake. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *